Bara Afrika lina utajiri mkubwa wa mifugo unaokadiriwa kuwa theluthi moja ya idadi ya idadi ya mifugo duniani. Japo idadi hii hutofautiana kutoka eneo moja hadi jingine, lakini kwa ujumla hili bara za wafugaji. Mifugo ni moja rasilimali muhimu za kilimo kwa watu wengi hasa vijijini na watu wenye kipato duni mijini hasa wanawake na wafugaji. Rasilimali hii hutoa mchango mkubwa wa kipato na husaidia kama hifadhi dhidi ya changamoto za kiuchumi na mabadiliko ya tabia nchi kwa kutoa mchango wa ajira, usalama wa chakula na lishe.

Sekta ya mifugo kwenye bara hili huchangia kati ya 30% na 80% ya pato ghafi la sekta kilimo kutegemeana na nchi kwenye uga wa 85% kwa nchini Somalia kufikia 80% nchini Djibouti na 47% nchini Ethiopia au 31% nchini Tanzania. Sekta hii kwa upande wa Afrika Mashariki huchangia zaidi ya dola billion 1 za Marekani(US$1 billion) kwa mwaka kupitia mauzo ya wanyama au nyama kwa nchi za Mashariki ya kati na Afrika ya Kaskazini.

Kimsingi, sekta hii hutegemea sana ufugaji wa ng’ombe, kondoo, mbuzi, punda, ngamia na kuku. Hata hivyo, ufugaji wa nguruwe unakua kwa kasi kubwa kusini mwa jangwa la Sahara kukiwa na kiwango kikubwa kwenye nchi za Burkina Faso, Ghana, Nigeria, Togo na Uganda. Ufugaji wa kuku na ulaji wa nyama nao umeshamiri. Kwa mfano Afrika Kusini ina idadi kubwa zaidi ya kuku na mzalishaji mkuu wa nyama ya kuku kwa zaidi metriki milioni 2.3 kwa mwaka, wakati nchi kama Senegal na Tunisia zikijitosheleza kwa mahitaji yake ya ndani.

NOTE: hapa utaweka pie chart PIE CHART inayoonesha; Ndege wa kufuga 61%, Nguruwe 1%, Ngamia 1%, Mbuzi 13%, Kondoo 12%, Ng’ombe 11%  Jamii ya Farasi. 1%

Chati; Idadi ya Mifugo 2018.

Chanzo: FAOSTAT 2019

Kwa mujibu wa ripoti ya Malabo Montpellier~2020; mifugo jamii ya ndege ilikuwa bilioni 2.3, mbuzi milioni 438, kondoo million 384, ng’ombe milioni 356, nguruwe milioni 40.5, ngamia milioni 31, jamii ya farasi milioni 38.

Nchi za Afrika Mashariki na Magharibi zinaongoza kwa ufugaji wa mbuzi lakini Afrika Mashariki ikiwa na wingi wa ng’ombe. Tafiti za hivi karibuni zinaonesha kuwa ufugaji wa ng’ombe unachukua sehemu kubwa ya ardhi kwenye nyanda za juu za Afrika Mashariki na nchi za Nigeria na Ethiopia. Nchi za Afrika Mashariki zina msongamano mkubwa mifugo kwa eneo dogo la ardhi.

Hali hii, inafanya bara hili kubuni njia endelevu za ufugaji. Ni kwa muktadha huu serikali na sekta binafsi zinaongeza mashirikiano ili kufikia azma hii.

Hapa nchini Tanzania, jitihada hizi zinaendelea pia japo siyo kwa kiwango hitajika. Ni kwa msingi huu kampuni yetu ya MALEMBO FARM inajikita sana kwenye kutoa ushauri na mafunzo kwa wafugaji, matumizi ya teknolojia, kushiriki majukwaa ya sera na kushirikiana na kampuni zenye maono kama yetu ndani na nje ya nchi kuimarisha sekta hii.

Kupitia jukwaa, nitakuletea uchambuzi wa kina kuhusu fursa Tanzania ilizonazo kwenye sekta, nafasi yake kwenye soko huru la biashara Afrika na hatua za kuchukua.

Tags:

Comments are closed

Subscribe To Our Free Farming Lessons

Subscribe To Our Free Farming Lessons

Join our mailing list to receive the latest news and updates from our team.

You have Successfully Subscribed!